Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Stellah Mutahibirwa. akizungumza kwenye michuano hiyo, amesema mashindano hayo yana lengo la kupinga vitendo vya ukatili na matukio mengine ya uhalifu eneo hilo.
(ACP) Stellah Mutahibirwa. amesema kwa kupitia fursa ya Polisi Jamii itasaidia kuiweka jamii karibu na polisi, jambo litakalowezesha kupata taarifa za uhalifu kwa urahisi na kuwaondoa wananchi hofu iliyojengeka kwa polisi.
Amesema wameandaa mashindano hayo ikiwa ni utaratibu uliopo chini ya IGP Camillus Wambura lengo likiwa kutoa elimu juu ya tabia hatarishi na vijana kuwa na afya bora kupitia michezo hivyo kuwaepusha vijana kuacha tabia za matumizi ya dawa za kulevya, bangi na ulevi ambavyo huchangia kuzorotesha uchumi wa nchi.
Mwenyekiti wa chama cha soka Mkoa Wa Singida (SIREFA ),Bw Hamisi Kitila amewapongeza polisi kwa kuanzisha michuano hiyo ambayo itachangia vijana kushiriki michezo.
![]() |
Maduka Saba wakisheherekea ubingwa kwa pamoja na Jeshi la polisi |
![]() |
Washindi Wa Tatu Timu Ya Minzani Fc wakiwa pamoja na Jeshi La Polisi |
![]() |
Waamuzi Wa Mchezo Wa Fainali ya Polisi Jamii Cup Singida Wakiwapamoja na jeshi la polisi |
![]() |
Picha Ya Kikosi Cha Maduka Saba(Bingwa) |

![]() |
Washindi Wa Pili Kwenye Mashindano Ya Polisi Jamii Cup .Msufini |
Na Mwandishi Wetu Singida
0 Comments