WAKINAMAMA mbalimbali kutoka Mkoa wa Pwani wamekuwa wakinufaika na kilimo cha nazi baada ya wawekezaji wengi kuwekeza katika bidhaa hiyo na kufanya kilimo hicho kupanda thamani.
Akizungumza na HabariLEO, mfanyabiashara wa kuuza na kubangua nazi, Khadija Mohamed amesema zao hilo limekuwa likipata umaarufu kutokana na watu wengi kutumia mafuta ya nazi kujipakaa.
Alimshukuru Mkurugenzi wa Active Mama, Ernestina Mwenda ‘Cocunut Lady’ kutokana na kuwaunga mkono kwa kununua nazi nyingi ambazo zinawasaidia katika kujikimu.
Alisema kampuni ya Active Mama imekuwa mstari wambele katika kuhakikisha inasaidia wakinamamawengi kwa kununua nazi katika maeneo yao nakufanya ubanguaji wa nazi hali ambayo inafanyainawapa ajira mara mbili.
“Kwanza tunauza nazi ambapo tumekuwa tukipatafedha za kutosha, lakini pia amekuwa akibangua nazina kufanya tupate ajira nyingine” alisema Khadija.
Ernestina alisema amekuwa akitumia nazi za asilikatika kutengeneza mafuta ya Active Mama, ikiwakama sehemu ya kuunga mkono kilimo cha nazi lakinipia kuifanya jamii kutotumia kemikali katika miili yao.
“Unapotumia mafuta ya nazi ya asili, unafanya ngoziyako ibaki katika ubora unaostahili, lakini piaunasaidia kilimo cha nazi kwa ndani ya nchi.
0 Comments