BILIONEA Mohamed al-Fayed, mzaliwa wa Misri ambaye mwanawe alikufa katika ajali ya gari na Princess Diana wa Uingereza, amefariki akiwa na umri wa miaka 94, familia yake imeeleza katika taarifa.
–
Al-Fayed, mmiliki wa zamani wa duka kuu la Harrods huko London na mmiliki wa klabu ya soka ya Fulham, alimpoteza mtoto wake Dodi Fayed katika ajali ya gari huko Paris na Diana mnamo 1997.
–
“Bi Mohamed al-Fayed, watoto wake na wajukuu wangependa kuthibitisha kwamba mume wake mpendwa, baba yao na babu yao, Mohamed, amefariki dunia kwa amani siku ya Jumatano Agosti 30, 2023,” familia yake ilisema katika taarifa iliyotolewa na klabu ya soka ya Fulham Ijumaa.
“Alifurahia kustaafu kwa muda mrefu na kufariki akiwa amezungukwa na wapendwa wake. Familia imeomba faragha yao iheshimiwe wakati huu.” familia hiyo ilisema.
–
Al-Fayed aliamini kuwa Dodi na Diana waliuawa katika njama iliyopangwa na Prince Philip, mume wa Malkia Elizabeth II.
0 Comments