Baba Ramsdale: Carragher kuwa na heshima

KAULI za kibaguzi za baadhi ya wadau wa soka duniani kwa wachezaji zinaendelea kuchukuwa sura mpya kwa wazazi wa wachezaji.

Wiki mbili zilizopita, Zoe Maguire, mama wa beki Harry Maguire alichukizwa na kauli za kibaguzi dhidi ya mtoto wake kufuatia kiwango kisichoridhisha cha mchezaji huyo wa Manchester United.

Katika muendelezo wa wazazi kuchukizwa na kauli hizo, Nick Ramsdale, baba mzazi wa kipa wa Arsenal, Aaron Ramsdale amechukizwa na kauli ya beki wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa michezo Skysport.

Katika mchezo wa EPL, Arsenal dhidi ya Spurs uliopigwa Jana Emirates, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta aliendelea kumpa nafasi kipa mpya David Raya na kumuacha benchi Aaron Ramsdale, wakati mpira ukiendelea kipindi cha kwanza, Ramsdale alimpigia makofi Raya baada ya kuokoa mpira ambao wengi hawakutegemea.

Kitendo cha kupiga makofi kilimfanya Carragher kutoa kauli: “Unajua mtu anapopoteza Oscar na kuanza kupiga makofi na kutabasamu kwa ajili ya mtu mwingine.” Kauli hiyo imetafsiriwa kuwa ya kibaguzi na kupelekea baba wa mchezaji huyo kutoa kauli.

“Wewe umekosa heshima onyesha daraja fulani vijana wangu.” Aliandika Nick.

Katika mchezo huo Arsenal ilipata sare ya pili msimu huu ya mabao 2-2 na hivyo kuwa na pointi 14.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments