KLABU ya Barcelona ina mpango wa kumsajili mashambuliaji kinara wa Manchester City na timu ya taifa ya Norway Erling Haaland ifikapo mwaka 2025 ambapo wanaamini dau la £150M litatosha kukamilisha usajili wa nyota huyo.
Barca wanamuona Haaland kama Mrithi sahihi wa mshambuliaji Roberto Lewandowski hivyo tayari hesabu zao zimeelekezwa kwa mfungaji huyo bora EPL msimu uliopita.
Kwingineko Barcelona bado wanatajwa kuwa katika mazingira mazuri ya kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji wa Manchester City, Bernado Silva, na kwa kulitambua hilo Manchester City wapo kwenye mazungumzo na nyota huyo ili kuweka kipengele cha £50m kwa timu inayomtaka Silva.
Imeelezwa kuwa miamba ya soka la Ujerumani Bayern Munich bado wana mkataba na kocha Julian Nagelsmann hadi mwaka 2026 licha ya kocha huyo kufutwa kazi na nafasi yake kuchukuliwa na Thomas Tuchel.
Taarifa zinaeleza kuwa licha ya mkataba huo Bayern hawatohitaji malipo yoyote kutoka kwa shirikisho la soka nchini Ujerumani iwapo watahitaji huduma ya kocha huyo kwenda kuinoa timu ya taifa ya Ujerumani.
Kwa sasa shirikisho hilo linamsaka mrithi wa kocha Hans Flick aliyefutwa kazi kutokana na mwenendo usioridhisha wa mabingwa hao wa kombe la dunia mwaka 2014.
0 Comments