CCM YARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WATAALAM WA KATA YA CHANG’OMBE

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chang’ombe, Bashiri Iddy ameridhishwa na utendaji kazi wa maafisa watendaji wa mitaa ya Kata ya Chang’ombe na kuwataka wachape kazi kwa kujiamini na kutoyumbishwa katika kutekeleza majukumu yao.


Kauli hiyo aliitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa Chilewa katika Kata ya Chang’ombe, Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Iddy alisema kuwa maafisa watendaji wanafanya kazi vizuri. “Watendaji wangu chapeni kazi kwa kujiamini, yale tunayoyasema na kuyaelekeza mkayatekeleze kwa weledi. Watendaji wa mitaa nawashukuru sana mnafanya kazi nzuri sana. 

Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Chilewa umesimama umetoa taarifa ya utekelezaji ya miaka minne yenye dira nzuri ya mtaa unaouongoza. Taarifa imetolewa imenyooka, sisi tutaendelea kuwaunga mkono. 

Afisa Mtendaji wa Kata ya Chang’ombe nakushukuru sana, kwa sababu bila wewe ofisi ya kata ingeyumba, endelea kutoa maelekezo kwa wenzako, wape ushirikiano jengeni sifa ya kazi katika kazi yenu. Mkimuangusha Diwani Fundikila kwenye taarifa zetu mmekiangusha Chama Cha Mapinduzi pia” alisema Iddy.

Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chang’ombe kinafanya ziara ya kikazi katika Matawi yote ya chama hicho kukagua uhai wa chama, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kuwashukuru wanachama wake kwa kuchagua uongozi wa CCM Kata ya Chang’ombe.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments