MSHAMBULIAJI wa PSG, Kylian Mbappe amepata jeraha la kifundo cha mguu lililomlazimu kufanyiwa mabadiliko katika mchezo wa Ligue 1 dhidi ya Marseille jana.
Mbappe amepata jeraha hilo baada ya kuchezewa rafu na Leonardo Balerdi hivyo kutolewa nje kabla ya mapumziko.
Bado hazijatoka taarifa rasmi za muda gani atakaa nje, ila imeelezwa huenda kuna hatihati kukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Newcastle United Oktoba 4.
Katika mchezo huo PSG iliifunga Marseille mabao 4-0 mabao yalfungwa na Achraf Hakimi, Randal Kolo Muani na mawili ya Goncalo Ramo
0 Comments