ARUSHA: MCHEZAJI chipukizi wa gofu kutoka Arusha, Shane Pandit amefanikiwa kutetea taji lake katika awamu ya tano ya mashindano ya Kimataifa ya Gofu ambayo yamechezwa katika uwanja wa Kill Gofu uliopo wilayani Arumeru, mkoani Arusha.
–
Shane mwenye miaka 14 anatoka klabu ya Arusha Gymkhana, ameng’ara na kushinda ubingwa huo mara ya pili mfululizo.
–
Zaidi ya wachezaji 100 wa gofu kutoka mataifa 18 duniani wamechuana vikali katika mashindano hayo ambayo lengo kuu ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
–
Bingwa huyo amekusanya alama 88 na kuibuka mshindi wa jumla ambapo pia mwaka 2022 katika mashindano hayo ya kimataifa yajulikanayo kama ‘Diplomatic Gofu ‘ aliibuka mshindi.
0 Comments