NAIBU WAZIRI MKUU DKT. BITEKO AIPONGEZA BoT KUANZA KUNUNUA DHAHABU

 Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko, (kushoto), akizungumza katika Banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT), alipofanya ziara kwenye Banda la Benki hiyo kujionea shughuli wanazofanya, wakati wa ziara yake ya kukagua Mabanda katika Maonesho ya Teknolojia ya Sekta ya Madini yanayoendelea kwenye Viwanja vya EPZ- Bomba mbili, leo Septemba 23,2023 Mkoani Geita.


Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko, (kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Victoria Msina (wa kwanza kulia), wakati wa Ziara ya Naibu Waziri Mkuu alipotembelea katika Banda la Benki hiyo, kwenye Maonesho ya Madini Mkoani Geita.

Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko, (kushoto) akimsikiliza Meneja Msaidizi, Upatikanaji na Usimamizi wa akiba ya Fedha za kigeni nchini, Dkt. Anna Lyimo (wa pili kulia), alipokuwa akielezea jinsi Benki hiyo ilivyowekeza katika sekta ya Madini kwa kuanza kununua Dhahabu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments