USHINDI au sare ya bila kufungana, itawapeleka Simba SC katika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya mchezo wa leo kuisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya Power Dynamos nchini Zambia. – Simba itarudiana na timu hiyo Septemba 30, Dar es Salaam. – Katika mchezo huo, wenyeji Dynamos walianza kutangulia kwa bao lililofungwa na Joshua Mutale dakika ya 29, bao hilo lilidumu hadi mapumziko. – Dakika ya 60 Clatous Chama alisawazisha bao hilo na kuwa 1-1, kabla ya dakika ya 75 Cephas Mulombwa kuifungia Dynamos bao la pili. – Dakika za mwisho Chama alifunga tena na ubao kusomeka 2-2. – Wakati huohuo Yanga imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya El-Merreikh ikiwa ugenini. – Mabao ya Yanga yalifungwa na Kenneth Musonda dakika ya 63 na Clement Mzize dakika ya 80. – Sare yoyote itawavusha Yanga kwenda hatua ya makundi.
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI
Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516
0 Comments