WADAU wa elimu jijini Arusha wameunga mkono mapendekezo ya serikali katika kuboresha mitaala ya elimu.
Wameeleza kuwa mabadiliko hayo yataleta mapinduzi katika sekta ya hiyo na maendeleo ya nchi kwani vijana wanaohitimu katika madaraja mbalimbali watakuwa na ujuzi utakawasaidia kuajiriwa au kujiajiri.
Mmoja wa wadau hao ambaye pia ni Mbunge wa jmbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo amesema elimu inayotolewa nchini hivi sasa imekuwa na changamoto kubwa kwa wahitimu kwani imekuwa ya nadharia zaidi kuliko vitendo.
Amesema hali hiyo inawajenga vijana wanaohitimu katika shule na vyuo kulazimika kuajiriwa tu.
Alisema mpango wa serikali kuboresha mitala ya elimu kwenda na wakati ni njia pekee ya kuwakomboa vijana kuondoka na kusubiri kuajiriwa na badala yake wanajikuta wakijiajiri kwa maslaji yao na nchi kwa ujumla.
Gambo alisema ili taifa liwe bora lazima liwekeze katika elimu hivyo ndivyo serikali inavyotaka kufanya kwa kubadilisha mitala ya elimu kwa vijana wanaohitimu katika vyuo mbalimbali.
” Tunataka vijana wanaohitimu wawe na elimu bora lengo ni kutaka kupata wataalamu wenye sifa zilizotukuka katika kuongoza nchi.” alisema Gambo
Aidha Gambo amewataka wazazi kuwa malezi mazuri wa kuwa karibu na watoto ili kujua mienendi yao ya kila siku watokapo shule.
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Royal, Fadhili Abrahaman alisema wanaunga mkono jitihada za serikali kutambua changamoto ya ajira nchini na kusema kuwa maamuzi ya serikali huenda ikawa mkombozi kwa Vijana wengi kujiajiri.
0 Comments