Wananchi Mtwara kicheko kulipwa fidia

WANANCHI mkoani Mtwara waliokuwa wanadai fidia ya mazao kutoka kwa Kampuni ya Utafiti wa Gesi na Mafuta (ARA Petroleum Tanzania) wameeleza kufurahishwa hatua ya Kampuni hiyo kuwalipa fidia yao bila kupitishia Benki.

Wakizungumza mara baada ya kupokea malipo ya fidia wananchi hao wameeleza kufurahishwa na utaratibu huo huku wakitaka utaratibu wa kulipa fidia kwa pesa mkononi utumike inapotokea wananchi kudai fidia.

“Utaratibu wa ulipaji nimeufurahia sana, na tena ningependa hata ulipaji wa nyuma ungefanyika kama huu, mpaka kufika leo asingekuwepo mtu yeyote anadai,” amesema Hamis Liwaka .

Liwaka amesema ulipaji wa pesa taslim hauna changamo zozote ambapo walifika na kupewa karatasi ya kusaini na Kisha kuingia chumba cha kupokelea pesa na kupata pesa yao na kuondoka.

“Huu utaratibu wa kupokea fidia yetu binafsi nimeupenda sana, huu ni tofauti na ule wa nyuma ambapo ilikuwa inamlazimu mwananchi awe na akunti benki ,na sio rahisi kupata hiyo akaunti ina gharama sana na usumbufu mwingi,” amesema Aziza Yusuf.

Mwakilishi wa Kampuni hiyo, Judith Kalugasha amesema Wananchi 203 Kati ya wananchi 4269 waliokuwa wanadai fidia ya mazao kutoka kwa Kampuni hiyo walishindwa kulipwa stahiki zao kwa muda kutoka na kutokuwa na akatunti benki ili kuwekewa hela zao.

Amesema Kampuni ya ARA Petroleum kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) walichukua baadhi ya maeneo ya Wananchi kwa ajili ya utafiti na gesi asilia eneo la Ntorya ambapo waliharibu mazao ya Wananchi.

Mjiolojia kutoka TPDC Patrick Kabwe amesema utafiti wa gesi asilia eneo la Ntorya ulifanyika mwaka 2021 na kumaliza October, 2022.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments