Kauli hiyo imetolewa Septemba 9,2023 na Mdau wa Maendeleo Bw. Ayubu Semvua katika mahafali ua shule ya msingi Turiani Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Bw. Semvua amesema ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha watoto wanaishi katika maadili mazuri kwani kunamjenga mtoto kukua kwa kutambua mema na mabaya.
Amesema malezi ya mtoto yanaanzia nyumba, hivyo wazazi wanajukumu la kusimamia mienendo ya watoto wao hasa kwenye masuala ya tabia ili kuepuka makundi hatarishi kwenye jamii inayotuzunguka.
Pamoja na hayo amewataka wahitimu kuepuka kujichanganya na makundi hatarishi ambayo yanaweza kusababisha kuingia kwenye vishawishi hatarishi.
Katika Mahafali hayo uongozi wa shule umempongeza mdau wa Maendeleo Iddy Azan kwa namna anavyochochea Maendeleo katika shule hiyo.
0 Comments