WAZIRI MKUU AKAGUA SOKO LA KIMATAIFA LA DAGAA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba ahakikishe anaweka utaratibu mzuri wa uendeshaji wa soko la kimataifa la mazao ya uvuvi la Magarini ikiwemo kuajiri mtumishi wa Serikali atakayesimamia makusanyo.


“Lete Afisa Mapato hapa badala ya kutoa ajira kwa vibarua; eneo hili litawasaidia kupata mapato mengi ambayo yatasaidia kuendesha soko hili ikiwemo kuweka taa za barabarani. Wavuvi wenu wahudumiwe na wasaidiwe ili waweze kufanya kazi zao kwa urahisi,” amesema wakati akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi huyo, Dkt. Peter Nyanja.

Ametoa wito huo leo (Jumapili, Septemba 24, 2023) wakati akizungumza na wananchi wa Magarini na wafanyabiashara mara baada ya kukagua bandari ya Magarini na Soko la Kimataifa la mazao ya Uvuvi la Katembe - Magarini lililopo kata ya Nyakabango, wilayani Muleba, mkoani Kagera.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali imeweka utaratibu kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kuwawezesha wavuvi kufanya shughuli zao kwa tija. “Rais Dkt. Samia ameweka nguvu ili kuwanufaisha wavuvi ikiwemo kununua boti 1,200 kwa ajili ya vikundi vya wavuvi ili kuwawezesha wavue mbali zaidi.

Katika mwaka fedha 2022/2023, soko hilo linalohudumiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania, Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Halmashauri ya Muleba lilizalisha tani milioni 26.96 za dagaa na samaki kutoka visiwa vya Bumbire, Maziga, Ikuza, Kerebe na Goziba.
 W
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuelekeza Meneja Bandari - Kanda ya Ziwa Victoria, Bw. Erasto Lugege afanye maboresho ya bandari ya Magarini kwenye eneo la jengo la abiria na gati.

Vilevile, amezitaka taasisi za Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya HIfadhi za Taifa (TANAPA) na Halmashauri ya Wilaya zikae pamoja na kupanga vizuri eneo hilo ili liwe kivutio.

“Malengo yetu ni kuongeza kituo cha TANAPA ili shughuli za utalii zianzie hapa kwenda kwenye hifadhi ya Rubondo badala ya kuzunguka hadi Chato,” alisema.

Akitoa taarifa yake, Meneja Bandari - Kanda ya Ziwa Victoria, Bw. Erasto Lugege alisema kwenye bajeti ya 2023/2024 wanatarajia kuboresha gati hilo ambalo lilifunikwa na maji tangu mwaka 2020 kutokana na mvua kubwa zilizonyesha kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia vifaa vya kufundishia, wakati alipokagua uboreshaji wa miundombinu kwenye Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), kilichopo kata ya kijiji cha Bushagara, Kamachumu mkoani Kagera, Mheshimiwa Majaliwa yupo mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi, Septemba 24, 2023. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Anthony Kasore. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi, wakati alipokagua uboreshaji wa miundombinu kwenye Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), kilichopo kata ya kijiji cha Bushagara, Kamachumu mkoani Kagera, Mheshimiwa Majaliwa yupo mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi, Septemba 24, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Kamachumu, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani humo, Septemba 24, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia nyavu haramu, zilizokamatwa, wakati alipokagua Soko la Kimataifa la Mazao ya Uvuvi la Katembe-Magarini, lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, mkoani Kagera akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani humo, Septemba 24, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia ghala, wakati alipokagua Soko la Kimataifa la Mazao ya Uvuvi la Katembe-Magarini, lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, mkoani Kagera akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani humo, Septemba 24, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi, wakati alipokagua Soko la Kimataifa la Mazao ya Uvuvi la Katembe-Magarini, lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, mkoani Kagera akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani humo, Septemba 24, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments