Ajali ya basi yaua 18

 

TABORA: Watu 18 wamefariki dunia, baada ya basi la abiria kugongana uso kwa uso na lori la mafuta wilayani Nzega, mkoani Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa Tabora, Richard Abwao, amesema ajali hiyo imetokea leo saa 4 asubuhi eneo la Uchama, Nzega ikihusisha basi la abiria mali ya Kampuni ya Alpha likiwa na abiria 60 wakielekea Dar es Salaam wakitokea jijini Mwanza.

Kamanda Abwao amesema chanzo cha ajali hiyo kwa taarifa za awali zinaeleza ni uzembe wa dereva la lori kutaka kulipita gari lingine bila kuchukua tahadhari.

Ameongeza  kuwa miongoni mwa waliokufa ni wanaume 13, wanawake 5 na wengine 36 wamejeruhiwa  idadi hii ni pamoja na watoto wadogo ambao miili yao ilipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.

Mkuu wa Wilaya ya Nzega Naitwapwaki Tukai amesema wamepokea miili 18 baadhi yao ni watoto wadogo kwa sasa wanafanya kazi kusaidia majeruhi kupata matibabu yanayohitajika kwa haraka sana iwezekanavyo.

Amesema kuwa serikali wilayani Nzega inafanya kila linalowezekana kuhakikisha matibabu yanapatikana kwa majeruhi wote.

Baadhi ya manusura walikuwa wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mji wa Nzega huku wengine wakikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Nkinga wilayani Igunga.

Kwa upande wake, Ofisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA) Nelson Mmari, amesema kuwa miongoni mwa abiria waliopanda basi hilo lililopata ajali, ni 49 waliokuwa na tiketi za kielektroniki jambo ambalo lilifanya iwe rahisi kutambulika.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments