MTWARA: WATU saba wamefariki dunia na wengine 22 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea Kijiji cha Kiwawa, Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Pili Mande amesema ajali hiyo ilihusisha basi aina ya Scania la Kampuni ya Saibaba, ambalo liligongana na basi dogo aina ya tata.
ACP Mande amesema chanzo cha ajali ni dereva wa basi ambaye alitaka kulipita gari kubwa la mizigo ambalo lilikuwa mbele yake na kukutana na basi dogo ambalo lilikuwa linatokea kwa mbele.
Kamanda amesema miongoni mwa waliofariki kuwa ni Lucas John (59) dereva wa Saibaba, Omary Abdallah (49) dereva wa basi dogo.
Amesema miili ya watu wengine watano haijatambuliwa na imehifadhiwa hospitali ya Kinyonga wilayani Kilwa. Majeruhiwa wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Kinyonga.
0 Comments