Arusha watakiwa kulipa wenyeviti wa mitaa posho zao

 


ARUSHA; Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amemwagiza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Juma Hamsini kuwalipa posho zao wanazodai Sh 100,000 wenyeviti wa serikali za mitaa 154 ya jiji hilo.

Mongella ametoa agizo hilo wakati wa kukagua miradi mbalimbali inayojengwa na Jiji la Arusha.

Amesema wenyeviti hao wanapaswa kulipwa fedha zao kila mwezi na amepata malalamiko ya kutolipwa fedha hizo kutoka kwa wenyeviti hao na kusisitiza walipwe fedha zao zote wanazodai, kwani ni watu muhimu.

Pia amesisitiza jiji hilo kuendelea kuwekwa taa za barabarani, ili kuwezesha wananchi kupata mwanga nyakati za usiku, kwani jiji hilo ni kubwa katika utalii.

“Arusha ndio kitovu cha taasisi za Afrika za kisheria na ni jiji la utalii, hivyo lazima kuwepo na taa, lakini pia kuongeza juhudi zaidi katika ukusanyaji wa mapato,” amesema.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Hamsini amesema atalipa wenyeviti hao fedha zao wanazodai na kusisitiza kuwa jiji hilo litaendelea kufungwa taa maeneo mbalimbali.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments