OFISA Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe amepigwa faini ya Sh milioni 1 na Bodi ya Ligi kwa kosa la kumkejeli mwamuzi Tatu Malogo kupitia mitandao ya kijamii.
–
Imeelezwa Kamwe alichapisha picha ya mwamuzi huyo katika ukurasa wake wa Instagram akiunganisha na wimbo wa Billnas uitwao ‘Maokoto.
–
Kitendo hicho kimetafsiriwa kumhusisha mwamuzi huyo na masuala ya rushwa.
0 Comments