KATAMBI AWAASA VIJANA KUJITAMBUA NA KUWA WAZALENDO

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amewaasa vijana  kujitambua na kuwa wazalendo katika kulijenga Taifa lao.  

Amesema maendeleo ya Taifa lolote yanahitaji vijana wanaojitambua, wanaofahamu historia ya nchi yao, wanaojali Afya zao, wakatambua wajibu wao, wakafanya kazi kwa bidii na wakawa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali.

Mhe. Katambi amebainisha hayo Oktoba 8, 2023 alipotembelea mabanda  ya vijana wajasiriamali ikiwa ni wiki ya vijana kitaifa  inayofanyika Mkoani Manyara na kukagua maendelea ya shughuli za mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2023..

Aidha, amesema Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imeandaa mazingira wezeshi na fursa za ajira kwa vijana  ili kutimiza malengo waliyojiwekea  ikiwa ni pamoja kutoa programu za kukuza ujuzi, mikopo kwa mtu mmoja mmoja ili wajikwamue kiuchumi.

Pia Mhe. Katambi  amekagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa Kwaraa na kuridhishwa nao ambapo amesema umefikia asilimia 95 na wapo tayari kumpokea Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge kitaifa 2023..

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments