KINDA wa FC Barcelona, Marc Guiu ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufunga bao kwenye mchezo wake wa kwanza wa La Liga akiwa na timu hiyo.
Ameweka rekodi hiyo baada ya kufunga bao kwenye mchezo dhidi ya Athletic Bulbao. Guiu alifunga bao dakika ya 80 ya mchezo, amefunga akiwa na umri wa miaka 17 na siku 291.
Bao hilo la pekee lililoifanya Barcelona iibuke na ushindi wa bao 1-0 imeifanya timu hiyo kuweka rekodi ya kuwa imechecheza michezo 8 mfululizo bila ya kufungwa dhidi ya Bilbao.
0 Comments