MABAO mawili yaliyofungwa na kiungo wa Yanga, Max Nzengeli katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Fontain Gate yamemfanya nyota huyo kufikisha mabao matano katika orodha ya wafungaji bora Ligi Kuu.
Max amefunga mabao hayo leo dhidi ya timu hiyo katika uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.
Kiungo huyo amefunga dakika ya 30 na 39 ya kipindi cha kwanza na mchezo kuisha kwa matokeo hayo.
0 Comments