“MNAMO Oktoba 29, mwaka 1923, miaka 100 iliyopita, Mara tu baada ya ushindi katika Vita vya Uhuru iliyofanyika (1919-1923), Bunge la Uturuki lilitangaza serikali mpya ya Uturuki kama “Jamhuri ya Türkiye”. Kiongozi katika vita vya Uhuru, Mustafa Kemal Atatürk alikua Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Türkiye siku hiyo hiyo.
“Leo tunasherehekea kwa furaha kumbukumbu ya miaka 100 ya Jamhuri ya Uturuki kuenzi ushindi na kutunza heshima ya Atatürk na askari wake waliofariki kwa ajiri ya uhuru wetu,” inaeleza taarifa ya Shirika la Uratibu la Uturuki (TIKA) kuhusu miaka 100 ya uhuru wa nchi hiyo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa katika kuadhimisha 100 ya kutangazwa Jamhuri ya Uturuki wametangaza programu kabamba ya mpira wa miguu.
“Katika kuadhimisha miaka 100 ya kutangazwa kwa Jamhuri ya Uturuki, tunayo furaha kutangaza mradi wa: “Miaka 100 Uturuki-Tanzania Msimbazi Football Field”, ambao ni moja ya matukio na miradi iliyoandaliwa Uturuki. Na duniani kote ilienda kwa jina la “Karne ya Uturuki”.
“Mradi huu kwa Ushirikiano na SaveHeaven Foundation na Samata Foundation, unaotekelezwa na Shirika la Uratibu na Ushirikiano la Uturuki TİKA utatoa fursa sawa za elimu ya michezo na nafasi kwa vijana wote wa jamii bila kujali dini, kabila wala jinsia, na ili tuweze kutoa fursa na kukuza vipaji vya vijana.
“Malengo yetu na mradi huo ni kuhakikisha shule za msingi, sekondari na vyuo vya soka vya Wilaya ya Ilala vinakuwa na eneo la zuri ili kuweza kuendana na mahitaji ya soka la kileo na kuwezesha kuibua vipaji vipya vya soka.
“Kama hatua muhimu ya “Karne ya Türkiye” katika historia ya taifa letu, tunasherehekea yote kwa pamoja watoto na vijana ambao ni mustakabali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa zawadi kutoka kwa mioyo ya watu wa Uturuki,” imesema taarifa hiyo.
0 Comments