Samia: India ni mshirika mkubwa katika Biashara

 

INDIA: RAIS Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania inajivunia ushirikiano uliopo na taifa la India kutokana na manufaa makubwa ya ushirikiano huo.
Rais Samia ameeleza hayo Oktoba 9, 2023 akiwa nchini India ambapo yupo katika ziara ya kikazi nchini humo.
Samia amesema mbali na mafanikio yaliyopatikana katika sekta mbalimbali lakini katika sekta ya biashara Tanzania inajivunia kukuwa kwa sekta hiyo.
“Tumekuwa tukifanya kazi kwa pamoja katika sekta mbalimbali, kuhusu biashara namba inaridhisha na imekuwa kwa kiasi kikubwa, na thamani ya miradi inaongezeka ,hii inaifanya India kuwa mwekezaji wa tatu mkubwa katika sekta ya biashara Tanzania.” amesema Rais Samia
Aidha Rais Samia amesema ziara hiyo ya nchini India ni kuonesha utayari wa Tanzania kuendelea na ushirikiano ulipo baina ya mataifa hayo mawili na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa karibu na taifa hilo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments