UNAAMBIWA kwa mara ya kwanza ndani ya miaka miwili, timu ya taifa ya San Marino imefunga bao kwenye michuano rasmi, licha ya kupoteza mabao 2-1 dhidi ya Denmark kwenye mchezo wa kufuzu Euro uliopigwa usiku wa leo.
–
Mshambuliaji wa Manchester United, Rasmus Hojlund, ndiye aliyeifungia Denmark timu iliyofuzu nusu fainali ya Euro 2020.
–
Lakini Alessandro Golinucci alisawazisha katika dakika ya 61, na kuamsha shangwe kali kutoka kwa mashabiki wa Marino.
–
‘Minnows’ San Marino hawakuweza kushikilia bomba, dakika ya 70 Yussuf Poulsen aliipa ushindi wa bao la pili Denmark na kufuzu Euro 2024.
–
Danes wanasalia nafasi ya pili katika Kundi H na wanaweza kufuzu kwa ushindi dhidi ya Slovenia katika mechi yao ijayo.
–
San Marino sasa wamepoteza mechi 83 kati ya 84 za kufuzu Euro, isipokuwa sare tasa dhidi ya Estonia mwaka 2014.
0 Comments