KIKOSI cha Simba SC kimewasili nchini kikitokea Misri ambako kilienda kwa ajili ya mchezo wa raundi ya pili wa African Super League dhidi ya Al-Ahly uliopiga jana Cairo na kuisha kwa sare ya bao 1-1.
Matokeo hayo hayakuwa na faida kwa timu hiyo kutokana na kuruhusu mabao mawili uwanja wa Mkapa katika mchezo ulioisha sare ya mabao 2-2 wiki moja iliyopita na hivyo Simba kuondolewa kwa kanuni.
Simba itaingia kambini kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu na ile ya Ligi ya Mabingwa itakayoanza mwezi Novemba.
0 Comments