DAR ES SALAAM: TANZANIA ni mwenyeji wa Mkutano wa pili wa Kimataifa wa Kutokomeza Ukeketaji ulio chini ya Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).
Mkutano huu unafanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, Dar es Salaam kuanzia leo Oktoba 09 hadi Oktoba 11, 2023
Zaidi ya washiriki 900 wanahudhuria Mkutano huu, kati yao 200 ni washiriki wa ndani na 700 ni kutoka Mataifa mengine.
Kauli mbiu ya Mkutano huu “Mabadiliko katika kizazi kimoja kwenda kingine ni muhimu katika kutokomeza vitendo vya Ukeketaji”
0 Comments