TCRA: Hatujakataza matumizi ya VPN bali…


DAR ES SALAAM: MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA) imesema taarifa yake iliyotolewa hivi karibuni  haijakataza matumizi ya VPN kama baadhi ya watu wanavyopotosha kupitia mitandao ya kijamii.

VPN ni programu tumizi inayomsaidia mtumiaji kujilinda hususani anapotumia mawasiliano ya Umma.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa TCRA, Rolf Kibaja imetoa maelezo hayo wakati Mamlaka hiyo ikiungana na taasisi nyingine  za mawasiliano duniani kuadhimisha ‘mwezi wa usalama mtandaoni’ huku akisitiza kuwa kilichoelezwa ni kwamba watumiaji wa VPN wanapaswa kutoa taarifa

“TCRA imetoa utaratibu kwa watumiaji wa VPN kutoa taarifa za matumizi ya VPN lakini haijazuia matumizi ya VPN. Watu wanaoshiriki kutoa taarifa kuhusu VPN wataendelea na shughuli zao kama kawaida kupitia VPN.

‘Ni muhimu kwa watumiaji wa VPN kutoa taarifa kwa kuwa kusajili huduma ya VPN ni kama kujisajili kwa namba ya simu. Nchi nyingi zilizoendelea duniani zimechukua hatua kama hizi kuimarisha usalama mtandaoni. Nchi hizi ni kama vile Uturuki, India, Belarus, Misri, China, na nchi nyingine. Ni muhimu kufahamu kuwa matumizi ya VPN nchini hayakatazwi bali yanapewa utaratibu rasmi,” Kibaha amefafanua.

Kibaja ameongeza kuwa kusema kwamba hakuna gharama yoyote ya malipo na kwamba hakuingilli masuala ya faragha wala usalama wa watumiaji husika endapo mtumiaji atatoa taarifa juu ya matumizi ya VPN.

“TCRA inaendelea kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuhakikisha usalama katika mtandao sambamba na watumiaji wa mtandao kuendelea kuwa salama. Asante sana…,” amehitimisha.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments