Wakulima kujiandikisha ugawaji wa mbolea Shinyanga

SERIKALI imeleta tani 3,278 za mbolea mkoani Shinyanga nakuwataka wakulima kujiandikisha na wale ambao walijiandikisha mwaka jana wahuishe majina yao ili kupata mbolea hiyo msimu wa kilimo 2023/2024.

Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme alipozungumza na watendaji wa kata, vijiji na mitaa wilayani Kahama kwa lengo la kuwakumbusha majukumu yao ya kazi na alieleza mbolea imekwisha fika kwa mawakala waliotambuliwa na serikali.

Mndeme aliwataka watendaji hao kuwa na daftari la kujiandikisha wakulima wote ili waeleze wanalima ekari ngapi, mazao gani ili serikali iweze kupata takwimu sahihi za wakulima na mazao wanayolima.

“Sasa hivi tumeelekeza mbolea ziwafikie wakulima kwenye maeneo yao karibu ninawahimiza wakulima kwenda kununua mbolea kwa mawakala hao ili walime bila wasiwasi nakupata chakula chakutosha”alisema Mndeme.

Mndeme alisema katika suala la upatikanaji wa mbolea kwa msimu wa mwaka 2023/2024 mpango ni mzuri tani 3,278 za mbolea zipo kwa mawakala wanaouza mbolea katika halmashauri zenu wakulima wahuishe majina yao haraka na wale bado wajiandikishe.

Mndeme alisema watendaji wanatakiwa kuwasaidia wakulima nakutoa namba zao za simu ili wanapopata changamoto na kushindwa kujieleza waweze kusaidiwa kwa kupigiwa mtendaji wa eneo husika.

Mndeme alisema sasa hivi mvua ipo karibu na wataalamu wameeleza kuna mvua nyingi msimu huu hivyo watumie fursa hiyo kwa tahadhari na kulima kwa bidii mazao yote ili wapate chakula cha kutosha kwenye kaya zao.

Baadhi ya watendaji wa kata waliohudhuria kikao hicho akiwemo Abeli Kahongwa kutoka kata ya Manase alisema wamejipanga kuwasaidia wakulima kwa kuwapa ushauri na kuwaandika kwenye dafrati ili kuwe na takwimu sahihi ndani ya kata pia.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments