Wanachuo watumiaji wakubwa dawa za kulevya

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kukevya (DCEA) Aretas Lyimo amesema kundi la vijana wasomi wa vyuo vikuu ndio linaloongoza kwa matumizi makubwa ya dawa za kulevya ikiwemo uchepushwaji wa kemilaki bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya.


Akizungumza Jijini Arusha katika halfa ya utiaji saini hati ya ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi katika kudhibiti uchepushwaji wa kemikali bashirifu na dawa tiba zenye athari za kulevya,Kamishna Jenerali Lyimo alisisitiza kuwepo kwa wimbi kubwa la Vijana wanaotumia kemikali hizo na kuharibika kiafya na kiakili.

Amesema vijana wasomi wanatumia dawa za kulevya na kuharibika kiafya na kushindwa kupata watoto na huko mbeleni wanaweza kubaki wazee pekee na kusababisha ajira za wasomi kuchukuliwa na wageni kwasababu ya ukosefu wa vijana wasomi
 
“Tumefanya utafiti mdogo na tumegundua vijana wasomi wanaongoza kwa matumizi ya dawa za kulevya na pia wengine wanasoma nchini Marekani na wengine vyuo vikuu hapa nchini na nchi nyinginezo,tutakosa wataalam wasomi badae sababu ya matumizi ya dawa tiba zenye asili ya madawa ya kulevya”
 
Amesema athari ya matumizi ya dawa hizi ni kubwa na mwisho wa siku wageni kutoka nje watashika nafasi hizi sababu hatuna wataalam katika fani nyinginezo sasa nawasihi nyie mnaouza kemikali muwe makini ili kudhibiti matumizi ya madawa haya.
 
Lakini pia taarifa ya hali ya dawa za kulevya Duniani kuanzia mwaka 2017 hadi 2021 zinaonyesha kuwepo kwa matumizi na usafirishaji haramu wa dawa tiba zenye asili ya kulevya mathalani dawa tiba zenye udhibiti maalum zilizokamatwa zikisafirishwa kwa njia haramu katika kipindi hicho.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments