WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wadau wa madini kujielekeza katika kutumia teknolojia za kisasa katika uchimbaji madini ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi zinazotokana na uchimbaji usio endelevu.
Hayo ameyasema leo Oktoba 26, katika Hafla ya Kufunga Mkutano wa Kimataifa wa Madini na Uwekezaji Tanzania (TMIF) wa mwaka 2023. Waziri Mkuu amefunga mkutano huo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
“Wadau waweke mikakati ya kuimarisha kaguzi katika masuala ya afya, usalama na utunzaji wa mazingira dhidi ya uharibifu unaoweza kuepukika katika shughuli za utafiti, uchimbaji na uchenjuaji wa madini”amesema Majaliwa
Hata hivyo Waziri Mkuu amesisitiza wadau mbalimbali waunganishwe na kuweka mikakati ya kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya madini kwa kufanya tafiti za madini mkakati, madini ya viwanda na madini ya metali.
Amesema kutokana na uwekezaji katika Sekta ya Madini kuhitaji mitaji mikubwa, hivyo ametoa rai kwa taasisi za kifedha kuweka mazingira nafuu ya taarifa za kutoa mitaji ya kuendeleza miradi ya madini.
Hata hivyo,Majaliwa amewataka wadau wa madini kuendelea kuunga mkono juhudi za dhati za Serikali ili kuiwezesha Sekta ya Madini kukua na kutoa mchango mkubwa kwenye Pato la Taifa.
Aidha Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwahakikishia wadau hao wa sekta hiyo kuwa, Serikali itazingatia ushauri na mapendekezo yaliyotolewa ili kuendelea kuboresha zaidi mazingira ya uwekezaji katika sekta ya madini nchini.
Kwa upande wake Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema Tanzania imebahatika kuwa mwenyeji wa mkutano huo kwa mara ya kwanza ulioonekana dunia nzima.
Amesema kupitia mkutano huo, wamepata fursa ya uwekezaji ,kujifunza mada mbalimbali za uchimbaji madini ya kimkakati na uchenjuaji wa madini.
Amesema mkutano wa mwaka jana ulikua na mada ya changamoto ya upatikanaji wa mitaji kwa wachimbaji wadogo ambapo changamoto hiyo imetatuliwa kwa kitolewa Sh. LPilioni 678 .
Aidha mkutano huo wa siku mbili umehudhuriwa na nchi 75 na wadau 1623 zikiwasilishwa mada 10 ukidhaminiwa na makampuni 14
0 Comments