YANGA SC wameingia mkataba wa miaka mitatu na Shirika la Bima la Taifa (NIC) wenye thamani ya Sh milioni 900 kwa ajili ya tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa timu hiyo.
Rais wa klabu ya Yanga, Hersi Said amesema Yanga itahakikisha mkataba huo utapewa thamani sahihi na kile kilichowekezwa na NIC.
“Mkataba huu utakuwa unalenga moja kwa moja kwa mchezaji bora wa mwezi, tunakuhakikishia mkataba huu utatoa thamani sahihi ya kile kilichowekezwa kwetu.” Amesema Hersi.
0 Comments