TIMU ya JKT Queens kutoka Tanzania imepata ushindi wake wa kwanza wa mabao 2-1 dhidi ya weneyji Atletico Footbal Club d’abidjan ya Ivory Coast kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa wanawake (CAFWCL).
Mabao ya JKT Queens yamefungwa na Alyah Fikiri na Winifrida Gerald huku Donisia Minja akiteuliwa kuwa mchezaji bora wa mechi (women of the match)
JKT Queens sasa ina pointi tatu hii ni baada ya kucheza michezo miwili na ilipoteza mechi ya kwanza dhidi ya Mamelodi Sundown Ladies.
Sasa mchezo wa mwisho JKT Queens inahitaji kupata ushindi dhidi ya Sporting Casablanca mchezo utakaochezwa Novemba 11,mwaka huu kujihakikishia nafasi ya kuingia hatua ya nusu Fainali ya Michuano hiyo.
0 Comments