NEC yateua Mbunge Viti Maalum

 

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imemteua Aziza Ally Sleyum kuwa Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge la Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhan Kailima imeeleza kuwa hatua hiyo inatokana na kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge ikiitaarifu Tume kuhusu kuwepo nafasi ya wazi ya ubunge kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, Bahati Ndingo.

Bahati alijiuzulu nafasi  hiyo ya ubunge Agosti 17 mwaka huu ili kuwania ubunge katika Jimbo la Mbarali, baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Francis Mtega kufariki dunia Julai Mosi, mwaka huu kwa ajali.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments