KUELEKEA mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga inayotarajiwa kupigwa Novemba 5, 2023 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es Salaam Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) limewataja marefa wanne watakaochezesha mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ofisa Habari Bodi ya Ligi, Karimu Boimanda amewataja marefa hao kuwa Ahmed Arajiga kutoka Manyara ndiye atakuwa mwamuzi wa kati na Mohamed Mkono kutoka Tanga atakuwa mwamuzi msaidizi namba moja huku Kassim Mpanga kutoka Dar es Salaam akiwa mwamuzi namba mbili.
Wengine ni Ramadhani Kayoko maarufu kwa jina la Etugru ambaye naye anatoka Dar es Salaam yeye atakuwa refa wa akiba huku Kamishna wa mechi hiyo inayotarajiwa kuanza majira ya saa 11 akitajwa Hosea Lugano kutoka Lindi.
0 Comments