ARUSHA; Mahakama ya Rufaa Chini ya Majaji, watatu leo inatarajiwa kusikiliza Rufaa iliyokatwa na Jamhuri kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kumwachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai ole Sabaya na wenzake wawili katika shitaka la wizi wa kutumia silaha na kujinyakulia zaidi ya Sh Milioni 2.7.
Kesi inasikilizwa na majaji watatu wakiongozwa na Mwenyekiti Jaji Jacobs Mwambegele, Jaji Ignas Kitusi na Jaji Leila Mgonya, ambapo upande wa Jamhuri umetoa sababu kadhaa za kisheria na kudai kuwa Mahakama Kuu ilikosea kumwachia huru Sabaya, kwani ushahidi ulithibitisha pasipo shaka kuwa mtuhumiwa alitenda makosa hayo.
0 Comments