Mwenyekiti wa UWT Ndg. Mary Chatanda (MCC) amesema kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) imeendelea kuboresha upatikanaji wa huduma za Afya ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025.
Mwenyekiti Chatanda ameyasema hayo leo Novemba 22, 2023 alipotembelea na kukagua Ujenzi wa jengo la mama na mtoto,jengo la upasuaji,jengo la kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mji KondoaUjenzi uliogharimu shilingi Milioni 900.
"Nimefurahishwa sana na Utekelezaji wa Mradi huu wa ukarabati wa Hospitali na nimeona hata wagonjwa wamefurahia huduma ya afya hivyo niwaombe wahudumu muendelee kuwahudumia wananchi kikamilifu katika maeneo yote ya huduma za afya ndani ya wilaya ya Kondoa ."




0 Comments