SIMBA SC imecheza mechi mbili Mfululizo bila kupata ushindi baada ya kushindwa kutamba dhidi ya Namungo FC kwa kutoka sare ya kufungana bao 1-1 mechi ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara mchezo uliopigwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Namungo FC walienda mapumziko wakiwa mbele ya bao moja lililofungwa na Mshambuliaji wake Realiantd Lusajo dakika ya 29.
Simba walisawazisha bao kupitia kwa Mshambuliaji wao Jean Baleke dakika ya 75 akimalizia pasi kutoka kwa Moses Phiri.
Kwa Matokeo hayo Simba SC imefikisha Pointi 19 na kubaki nafasi ya tatu wakicheza mechi 8 wakilingana Pointi na Azam FC waliocheza mechi 9 huku Yanga SC wakiendelea kukaa kileleni mwa Msimamo wakiwa na Pointi 24 wakicheza mechi 9.
0 Comments