ALGERIA: Kikosi cha Yanga leo kinatupa karata yake ya kwanza kwenye hatua ya makundi Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika watakapokuwa wageni wa Cr Belouizdad ya Algeria katika mchezo wa kundi D, utakaopigwa Uwanja wa 5 July 1962 nchini Algeria kuanzia saa nne usiku.

Yanga wanaingia kwenye dimba hilo wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda mchezo wa mwisho waliocheza katika uwanja huo dhidi ya USM Alger katika fainali ya kombe la shirikisho msimu uliopita walipoibuka na ushindi wa 1-0 licha ya kwamba hawakutwaa ubingwa wa michuano hiyo.

Mchezo mwingine utakaopigwa leo Pyramid ya Misri itawavaa Tp Mazembe ya DR Congo.
0 Comments