Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT, Mary Chatanda na msafara alioambata nao wamejikuta katika Simanzi nzito mara baada ya kumuona Mama aliyejifungua saa chache mara baada ya kuokolewa kwenye tope ambalo lilikuwa limemuonea mwili mzima na kumsomba mita kadhaa.
Akizungumza jana alipomtembelea Mwanamke huyo katika  Kituo cha Afya Gendabi mahali  ambapo ndipo kulikuwa  na Maafa makubwa kufuatia mafuriko yaliyotokea mara baada  ya Mlima Hanang kupasuka.
"Nimeshindwa kujizuia mimi kama Mama nikajikuta nalia kwa uchungu kuona Mwanamama  huyu ambaye  alisombwa na tope na kuweza kuokolewa  kwenye tope hilo  na kufikishwa hospital masaa mawili baadaye kujifungua  salama
Mtoto wa kiume  3/12/2023 kwa kweli nimelia uchungu  baada ya kusikiliza  simulizi za Mama huyu namna alivyohangaika kuokoa watoto wake wawili na huku mjamzito wa miezi tisa hakika hakuna kama Mama . Namshukuru  sana Mungu kutenda maajabu na kumuwezesha Mama huyu kujifungua  salama na mtoto yupo Salama  na ameitwa Mussa ." 
Aidha Mwenyekiti  amesema  Jumuiya itafanya jitihada kuhakikisha wanamuongezea  mahitaji ya kutosha 
Mama huyo ambaye kwa sasa yeye na familia wanalala hospitali kutokana na kukosa Makazi baada ya makazi yao kuharibiwa vibaya kutokana na mafuriko ya matope yaliyoikumba  baadhi ya maeneo ya wilaya ya Hanang .




0 Comments