Dk Ndumbaro apokea hati uwanja utakaopigwa Afcon

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro ametembelea na kukagua eneo la Olmoth Jijini Arusha, eneo ambalo litajengwa uwanja mpya wa mpira wa miguu wenye uwezo wa kuchukua watazamaji elfu 30 na utakaotumika katika michuano ya AFCON 2027.

Dk Ndumbaro ametumia wasaa huo kutoa maelekezo kwa wale wote ambao maeneo yao yatachukuliwa kutoa ushirikiano kwani fedha za fidia zipo na ametoa rai kwa yeyote yule anayefikiria kuleta mgogoro kwenye eneo hilo atashughulika naye.

“Mtu yeyote ambaye anayefikiria kuleta mgogoro kwenye eneo hili mtangazeni kuwa ni adui wa Umma, awe mtumishi wa Umma au awe mtu binafsi huyo ni adui wetu, tupambane nae, tushughulike naye.”amesema

Ametumia wasaa huo kumtaka meneja TANESCO Mkoa wa Arusha kufikiria kuleta umeme katika eneo hilo kwani Januari Kazi itaanza rasmi.

Amemtaka meneneja wa AUWSA kufanya utaratibu wa huduma ya Maji ya uhakika katika eneo la Uwanja, amewataka pia amewataka TARURA na TANROADS kuboresha Barabara inayoelekea eneo Uwanja utakapojengwa

Amesema kwa mujibu wa CUF wamepewa miezi24 Ujenzi ukiwa umekamilika hivyo inabidi wawakabidhi Uwanja CUF Disemba 2025.

sambamba na hilo Ndumbaro amepokea hati ya eneo hilo lenye ukubwa wa hekari 39 iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella ambaye amebainisha kuwa hati ya sehemu ya eneo lililobaki itakabidhiwa kwa Wizara kabla ya mwezi Machi, 2024.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amesema wao kama viongozi walivyokubaliana na wananchi pia kwamba eneo hilo linatoa Ekari 82 na Serikali itakabidhiwa hati

Mongella ameeleza kama Mkoa watahakikisha kabla ya Mwezi wa tatu Eneo lote la Ekari 82 limekabidhiwa hati kwa Serikali

Nae Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Juma Hamsin amesema eneo lililoagizwa na Mkuu wa Mkoa ni Ekari 83, na msimamo wa kuleta kiwanja Arusha ni Msimamo wa Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan hivyo kama Jiji la Arusha hawapo tayari kumwangusha

Hamsin amesema Ekari za mwazo zilizotolewa hati kwa Wizara ni 39 na zilizobaki ni 44 ambazo zipo kwenye Maandalizi hivyo Kama Mkurugenzi ametenga Bilioni 2.5 kwa ajili ya kulipia Fidia kwa wale watakao takiwa kupisha katika eneo hilo

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments