Kamati za maafa mikoa, wilaya jipangeni na ELNINO

MANYARA: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama ametoa wito kwa kamati za maafa za mikoa na wilaya nchini kote hasa kwa mikoa 14 iliyofanyiwa utabiri wa mvua za Elnino kujipanga kwa kuzingatia maelekezo waliyopewa kwani ni jukumu lao kutoa huduma ya haraka maafa yanapotokea.

Amezungumza hayo wakati wa kupokea misaada ya vifaa vya ujenzi ikiwemo mabati, mabomba na madawa kutoka kwa dhehebu la Bohora waliofika hii leo katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang kukabidhi misaada hiyo kwa wahanga wa maporomoko ya matope na magogo yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha katika Mlima wa Hanang.

Sambamba na hilo amewataka Wenyeviti wa kamati za maafa mikoa na wilaya kusimamia maelekezo yaliyopewa kwani shauku ya Serikali ni kuona Kila Mwenyekiti anakuwa kipaumbele kutekeleza waliyo kubaliana ili kusiwepo na uharibifu mkubwa wa miundombinu.

Pia amesema swala la kwanza kulipatia kipaumbele ni ulinzi wa uhai wa wananchi katika maeneo, ulinzi wa mali zao pia kuhakikisha huduma za kijamii zinakuwepo ikiwemo maji safi na salama, miundombinu ya umeme, zahanati,vituo vya afya na hospitali.

Jenista ameelekeza Kwa maeneo ambayo wanaona kuzidiwa nguvu watoe taarifa kwenye kamati ya maafa taifa

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments