Kaya 1,150 zapoteza makazi Katesh

 Hanang, Kaya 1,150 zenye watu 5600 zimepoteza makazi yake kwenye mji mdogo wa Katesh, na vitongoji vya karibu vya Jorodom, Ganana, Katesh na Dumbeta pamoja na Vijiji vya Gendabi, Sarijandu, Arukushay na Sebasi, wilayani Hanang, mkoani Manyara.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali, Mobhare Matinyi, hadi kufikia leo Desemba 5, 2023, saa 1:00 asubuhi, jumla ya majeruhi 117 walikuwa wameshapokelewa katika Kituo cha Afya Gendabi, Hospitali ya Wilaya ya Hanang (Tumaini) na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.

“Kati ya majeruhi hawa 18 hawakuwa na hali nzuri na walihamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara kwa matibabu zaidi, ambapo mmoja kati yao alifariki dunia siku moja baadaye, tarehe 04 Desemba, 2023, saa 4:00 usiku.

“Majeruhi wengine 17 bado wanaendelea na matibabu hospitali hapo. Majeruhi wengine 74 (ambao hawakupelekwa hospitali ya mkoa) bado wanaendelea kupata huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Hanang (Tumaini) na Kituo cha Afya Gendabi mjini Katesh. Na majeruhi waliotibiwa na kupata nafuu hatimaye kuruhusiwa kurejea nyumbani ni 25.

“Mchanganuo wa majeruhi 117 hadi kufikia asubuhi 05/12/2023 ni: Watu wazima 61: (Wanaume 30; wanawake 31). Watoto ni 56: (Wanaume 27; wanawake 29).

“Jumla ya miili 65 ilipokelewa na kuhifadhiwa katika Kituo cha Afya Simbay, Kituo cha Afya Magugu, Hospitali ya Dareda, Hospitali ya Mji wa Babati, Hospitali ya Wilaya ya Hanang (Tumaini), na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.

Mchanganuo wa vifo 65 vya marehemu waliopokelewa hadi kufikia asubuhi 05/12/2023 ni: Watu wazima 41: (Wanaume 15; wanawake 26). Watoto ni 24: (Wanaume 10; wanawake 14),” amesema Matinyi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments