Kinana awatuliza waathirika wa maafa Hanang

MANYARA: MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, amewahakikishia wananchi wilayani Hanang Mkoa wa Manyara hususani waliokumbwa na janga la mafuriko, kwamba maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, yatatekelezwa kikamilifu.
Kinana ameyasema hayo leo Desemba 4, 2023 alipowatembelea waathirika wa mafuriko hayo katika baadhi ya vijiji vya Wilaya ya Hanang.
Kinana amewatembelea na kuwafariji wananchi waliopoteza ndugu zao na waliojeruhiwa na kulazwa hospitalini kutokana na janga hilo ambapo amewapa pole na kuwaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments