MAKONDA AWAOMBA VIONGOZI WA DINI NCHINI KUENDELEA KUDUMISHA USHIRIKIANO KWA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Paul Christian Makonda, amewashukuru na kuwaomba Viongozi wote wa Dini nchini, kudumisha ushirikiano kwa viongozi wa Chama na Serikali, kwa kushauri na kutoa miongozo itakayowasaidia kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa haki na ufanisi ili kugusa matumaini yao kwenye nyanja mbalimbali za maendeleo nchini.


Mwenezi Makonda amesema hayo alipokwenda kumuona na kumsalimia Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, Mhashamu Baba Askofu Flavian Matindi Kassala, ofisini kwake, jimboni, mtaa wa Kambarage 14, mjini Geita, leo Alhamis, Disemba 28, 2023, ukiwa ni mwendelezo wa utaratibu wale wa kwenda kuwaomba ushirikiano, ushauri na miongozo mbalimbali viongozi wa kiroho wa madhehebu ya dini mbalimbali nchini, pamoja na makundi mengine ya kijamii, utakaomsaidia katika utekelezaji wa majukumu yake.

Kwa upande wake, Mhashamu Baba Askofu Kassala, pamoja na kumtakia kila la heri, amemhakikishia Mwenezi Makonda kuwa viongozi wa Dini wataendelea kutoa ushirikiano wao katika kuiombea Nchi, kuwashauri Viongozi na kuwapatia miongozo mbalimbali itakayowasaidia kuendelea kuwa watumishi bora wa wananchi, wanapotekeleza majukumu yao ya kuiongoza nchi kwa haki na upendo ili pia kudumisha umoja na mshikamano Kiongozi mwa Watanzania.

Aidha, Kwa pamoja wamefanya maombi ya kuliombea Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuendelea kuwa na Afya njema ili kuendelea kulitumikia Taifa letu la Tanzania.

Huu ni muendelezo wa Ziara za Mwenezi Makonda katika kuwatembelea Viongozi mbalimbali wa Dini Nchini.







TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments