TIMU ya Manchester United imeaga michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kumaliza kundi A ikiwa na pointi nne, ambazo zimeshindwa kuwavusha kwenda 16 bora.
Katika mchezo wa leo dhidi ya Bayern Munchen ulioisha kwa United kufungwa bao 1-0, timu hiyo ilihitaji ushindi wowote kisha Copenhagen na Galatasaray wamalize kwa sare ila mambo yakawa tofauti baada ya Copenhagen kushinda bao 1-0.
Kwa matokeo hayo, Bayern Munchen imeenda 16 bora ikiwa na pointi 14, na Copenhagen ikiwa na pointi 8.
United ilianza kundi hilo kwa mchezo dhidi ya Bayern ambapo waliofungwa mabao 4-3, kisha wakafungwa tena dhidi ya Galatasaray mabao 3-2.
Mchezo wa tatu dhidi ya Copenhagen, United walishinda bao 1-0, katika mchezo wa marudiano dhidi ya timu hiyo, wakapoteza tena mabao 4-3. United walipata sare ya mabao 3-3 dhidi ya Galatasaray mchezo wa marudiano.
Katika mchezo wa leo, bao la Bayern limefungwa na Kingsley Coman dakika ya 70.
0 Comments