Mchengerwa atoa maagizo kwa Wakurugenzi Halmashauri

SIMIYU: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amesema hatamvumilia Mkurugenzi yeyote wa halmashauri ambayo ataitia aibu serikali na kuifanya itukanwe kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Mchengerwa ametoa kauli hiyo baada ya kufika katika shule ya msingi Mwamashimba iliyopo wilayani Meatu mkoani Simiyu alioenda kukagua utekelezaji wa agizo lake.

Mchengerwa alitoa wiki mbili kwa uongozi wa mkoa na wilaya kufuatia taarifa ya watoto kukaa chini kwa kukosa madawati pamoja na Serikali kujenga shule nzuri.

“Kiongozi yeyote kwenye mamlaka za serikali za mitaa kwenye eneo lake ambaye anakwenda kuitia aibu Serikali mpaka tuandikwe na kutukanwa kwenye magazeti na kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kutotekeleza wajibu wako nitachukua hatua za kuwasimamisha kazi, ” amesema na kuongeza

“Nilimwambia RC Dk. Yahaya Nawanda kuwa leo nitaondoka na Mkurugenzi (Athuman Masasi) lakini nimekuhurumia kwa kuwa ni mgeni. Niwaambie wakurugenzi wa halmashauri kote nchini kuwa pale Serikali itatukanwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kwasababu umeshindwa kutekeleza majukumu nitachukua hatua dhidi yao.”

Amesema kiongozi bora ni yule ambaye anabeba matatizo ya wananchi kwenye mionyo yao na kutatua matatizo ya wananchi.

“Nchi hii haiwezi kujengwa na Rais pekee yake bali kwa kuwashirikisha wadau wa mandeleo.

Utoafuti kati ya kiongozi na mtu wa kawaida ni matendo yako namna ambayo umeshiba kero za wananchi, namna ambavyo unakwenda kutatua kero za wananchi.”

Amesema kama watendaji wa halmashauri wakiwamo wakurugenzi watafanyakazi kwa kungalia masilahi ya wananchi, kuangalia matatizo ya wananchi katika maeneo yao na kuyapa kipaumbele namba moja katika kuyamaliza.

“Watoto wanakaa chini, chukueni hatua msisubiri Rais aone kwenye vyombo vya habari wakati mnamapato ya ndani, kweli mimi (waziri) niwe Dodoma niagize kununua madawati 70 kwenye eneo lako?”

Mchengerwa pia aliwataka wakuu wa mikoa kwenda kuzungumza na watendaji walio chini yao kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kufubiri kupelekewa bajeti na kuwataka kujiongeza na kuwa wabunifu.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Athuman Masasi alikiri na kuomba msamaha kushindwa kupata taarifa sahihi kutoka kwa wasaidizi wake na kusisitiza kuwa halmashauri singeshindwa kutoa fedha za kununua madawati kutoka kwenye mapato ya ndani.

Awali, Mkuu wa Shule ya Msingi, Mwamashimba iliyopo wilayani Meatu, Mwita Manko alisema shule imepokea madawa 100 na kufanya sasa shule hiyo yenye wanafunzi 485 kuwa na jumla ya madawati 165 na meza sita za walimu hivyo kufanya shule kutokuwa na upungufu wa samani.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments