TANGA: Rais Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi kwa ajili ya sikukuu za mwisho wa mwaka kwa vituo 14 vya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu pamoja na makazi ya wazee mkoani Tanga
Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Rais Samia Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba amesema zawadi hizo ni kwa ajili kuwakumbuka makundi hayo ili nao waweze kusherehekea sikukuu .
“Rais ametoa zawadi hizo kwa makundi hayo maalum yaliyopo kwenye wilaya nane za mkoa huu ili nao wafurahie sikukuu kama sehemu ya jamii nyingine”amesema RC Kindamba.
Hata hivyo Mkuu wa mkoa ametoa rai kwa jamii kupenda kutoa mahitaji ikiwemo na kuwajali makundi ya watu wanaoishi kwenye mazingira magumu ili kudumisha amani umoja , upendo na mshikamano.
Jumla ya walengwa 334 waliopo kwenye vituo 14 ikiwemo makazi ya wazee wasiojiweza yaliyopo Mwanzange jijini Tanga wameweza kupatiwa zawadi hizo
Kila kituo kimepewa mbuzi mmoja , Mchele Kg 50 , Mafuta ya kupikia lita 10 sabuni katoni moja , maharage Kg 10 na sukari Kg 10.
0 Comments