Sasa ni New Amaan Sports Complex

 

ZANZIBAR: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi ameridhia ushauri wa kuubadili jina Uwanja wa Amaan na  kuitwa  “New Amaan Sports Complex” wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya uwanja huo uliofanyika Desemba 27, 2023.

Rais Mwinyi ameridhia ushauri huo uliotolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro alipokua akitoa salamu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuufanya uwanja huu kuwa wa kisasa na wenye viwango vya kimataifa, mimi naomba niubadilishe jina uitwe New Amaan Stadium” alisema Dk. Ndumbaro.
Hafla ya Uzinduzi wa Uwanja huo ilipambwa na Burudani mbalimbali ikiwemo Muziki na mechi ya mpira wa miguu ya kirafiki baina Kilimanjaro Stars na “Zanzibar Heros ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments