SIREFA YAPITISHA BAJETI YA MILIONI 55 KWA MWAKA 2024/2025

                        

Viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu  Mkoa wa Singida - SIREFA wametakiwa kuacha kuwa na makundi ndani ya Chama hicho ili kuleta maendeleo katika Sekta ya Mpira Mkoa wa Singida.

Diwani wa Kata ya Kindai OMARY KINYETO ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini SIREFA alisema hayo Mkoani Singida wakati akifunga Mkutano wa Mwaka wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida SIREFA 

KINYETO alisema kuwepo kwa Makundi ndani ya Chama cha Mpira yasiyo na msingi yanasababisha kurudisha nyuma na kuharibu taswira ya Mpira mkoa wa Singida.

Hata hivyo Kinyeto aliishukuru serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake wa kuiinga mkono Timu ya Taifa na kusababisha timu hiyo kushiriki mashindono ya Afcon nchini Ivory Coast.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu - SIREFA Mkoa wa Singida HAMIS KITILA alisema wataendelea kuweka mazingira mazuri ya michezo ili kuhakikisha Sekta ya Michezo inaleta Ajira kwa vijana.

KITILA alisema pia wataendelea kusimamia mchezo kwa kufuata kanuni na sheria za Mpira kwa lengo la kutoa haki katika michezo yote inayofanyika Mkoa wa Singida.

Alisema kwa mwaka ujao watatia nguvu zaidi kwenye Ligi za Vijana ili kuhakikisha Vijana wengi wanapata fursa za kwenda kucheza mashindano mbalimbali ndani na nje ya chini.

Kwa upande wa mashindono ya Mpira wa Miguu ngazi ya wanawake, KITILA aliwataka viongozi kuhakikisha wanasimamia Ligi za Wanawake ili Mkoa wa Singida uwe na Timu ya Wanawake inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania kwa upande wa Wanawake.

Aidha aliwashukuru Viongozi wa Manispaa ya Singida kwa kuendelea kuunga juhudi zinazofanywa na Chama cha Mpira kwa hali na mali kwa lengo la kuleta maendeleo kwenye Mpira.

Hata hivyo KITILA aliwataka wajumbe kuifanya SIREFA kuwa Taasisi inayojitegemea kwa kuwa na watu ambao wataisimamia kwenye mipango ya kuinua Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Wanawake Mkoa na Meya wa Manispaa ya Singida YAGI KIARATU aliwashukuru wajumbe kwa kuendelea kufuata kanuni na sheria za Mpira, hali iliyosaidia kutokuwepo kwa malalamiko mengi kwenye Chama cha Mpira Singida.

KIARATU alisema wilaya ambazo bado hazijazingia kwenye chama cha Mpira zihakikishe zinaingia kwenye chama ili kuleta maendeleo ya Mpira katika Wilaya hizo.

Aidha KIARATU aliwata viongozi wa Chama cha Mpira Singida kusimamia maadali, na kuwaonesha njia nzuri za kupita ili vipaji vyao vionekane na viweze kuwasadia.

Katika Mkutano huo wajumbe wa Mkutano huo wamepitisha Bajeti ya Milioni 55 zitakazotokakana na vyanzo mbalimbali vya SIREFA na zitakazotumika kuendesha shughuli mbalimbali za Mpira Mkoa wa Singida.

Wajumbe wa Mkutano huo, wao waliomba viongozi wa Chama cha Mpira Mkoa wa Singida kuwa na ushirikiano mzuri kwa lengo la kuleta maendeleo ya Mpira.





















 .....MWISHO.....

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments