Tanzania yatoswa waamuzi AFCON

CAIRO: Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetangaza majina 68 ya waamuzi watakaosimamia michezo ya Michuano ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika mwakani nchini Ivory Coast.
Katika waamuzi hao 68 waliotangazwa 26 ni waamuzi wa kati, 30 ni waamuzi wasaidizi wakati waamuzi 12 ni wa VAR.
Kwenye orodha hIyo hakuna jina la mwamuzi kutoka Tanzania huku majirani Kenya wakifanikiwa kupeleka waamuzi katika michuano hiyo mikubwa Afrika.
Mwamuzi, Salima Mukansanga kutoka Rwanda ambaye kwasiku za hivi karibuni amejitambulisha katika ulimwengu wa kandanda kutokana na uhodari wake wa kuzimudu vyema sheria za mpira wa miguu, amepenya tena katika michuano mingine mikubwa baada ya kutamba katika kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar.
Ikumbukwe Michuano ya Afcon inatarijiwa kuanza January 13 hadi February 11, 2024 nchini Ivory Coast na Tanzania ni miongoni mwa mataifa 24 yatakayoshiriki mitanange hiyo nchini Ivory Coast.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments